عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنين رضي الله عنها زَوْجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «يَا عَائِشَةُ إِنَّ اللهَ رَفِيقٌ يُحِبُّ الرِّفْقَ، وَيُعْطِي عَلَى الرِّفْقِ مَا لَا يُعْطِي عَلَى الْعُنْفِ، وَمَا لَا يُعْطِي عَلَى مَا سِوَاهُ».
Kutoka kwa Aisha Mama wa Waumini radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, mke wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema: "Ewe Aisha, hakika Mwenyezi Mungu ni Mpole anapenda upole, na hutoa malipo katika upole ambayo hayatoi katika ususuwavu (ukali), na wala hatoi kwa mengineyo".
‘Ā’ishah, the Mother of the believers (may Allah be pleased with her) and wife of the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him), reported that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "O ‘Ā’ishah, indeed, Allah is gentle and He loves gentleness, and He gives for gentleness what He does not give for violence and what He does not give for anything else."
Himizo juu ya upole na katazo la ukali.
Thamani ya nafasi ya upole katika tabia njema zote.
Mtu mpole anastahiki sifa nzuri na malipo makubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Amesema Assi-ndi: Ukali ni kinyume cha upole, yaani mwenye kuwaita watu kuja katika uongofu kwa upole na kwa huruma ni bora kuliko yule anayewaita kwa ugumu na ukali ikiwa mahali hapo panakubali mambo yote mawili, lau kama si hivyo basi achague kinachoendana na mahala, na Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi zaidi wa uhalisia wa hali.