Nyuma

Bismillaahi Arqiika, Min kulli shai-in Yu-udhiika, min sharri kulli nafsin Au Aini Haasidin, Allaahu yash-fiika, bismillaahi Arqiika" Yaani: Kwa jina la Mwenyezi Mungu ninakuombea, kutokana na kila kitu kinachokuudhi, na kutokana na shari ya kila nafsi au jicho la hasidi, Mwenyezi Mungu atakuponya, kwa jina la Mwenyezi Mungu ninakusomea

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ رَضيَ اللهُ عنه: أَنَّ جِبْرِيلَ أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: يَا مُحَمَّدُ اشْتَكَيْتَ؟ فَقَالَ: «نَعَمْ» قَالَ: «بِاسْمِ اللهِ أَرْقِيكَ، مِنْ كُلِّ شَيْءٍ يُؤْذِيكَ، مِنْ شَرِّ كُلِّ نَفْسٍ أَوْ عَيْنِ حَاسِدٍ، اللهُ يَشْفِيكَ بِاسْمِ اللهِ أَرْقِيكَ».

Kutoka kwa Abuu Saidi Al Khudri -radhi za Allah ziwe juu yake-: Ya kwamba Jibril alimjia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Ewe Muhammad umetekesa kwa maumivu? Akasema: "Ndiyo" Akasema: "Bismillaahi Arqiika, Min kulli shai-in Yu-udhiika, min sharri kulli nafsin Au Aini Haasidin, Allaahu yash-fiika, bismillaahi Arqiika" Yaani: Kwa jina la Mwenyezi Mungu ninakuombea, kutokana na kila kitu kinachokuudhi, na kutokana na shari ya kila nafsi au jicho la hasidi, Mwenyezi Mungu atakuponya, kwa jina la Mwenyezi Mungu ninakusomea.

Abu Sa‘īd (may Allah be pleased with him) reported: Gabriel came to the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) and said: O Muhammad, have you fallen ill? He said: "Yes." So Gabriel said: " Bismillāhi arqīk, min kulli shay’in yu’dhīk, min sharri kulli nafsin aw ‘aynin hāsidin, Allāhu yashfīk, bismillāhi arqīk (In the Name of Allah, I recite a prayer (Ruqyah) over you, from everything that harms you, from the evil of every soul or the eye of an envier. May Allah cure you. In the Name of Allah, I recite a prayer (Ruqyah) over you)."

Kufaa kuelezea maradhi ikiwa kama ni kuelezea uhalisia wa hali, na si sehemu ya kunung'unika na kulalamika.

Inafaa kusoma Ruqya kwa sharti zifuatazo: 1- Iwe kwa Qur'ani au kwa kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu na dua za kisheria. 2- Iwe kwa lugha ya kiarabu, au kwa maneno yanayoeleweka maana yake katika lugha zingine. 3- Aamini kuwa Ruqya haiathiri yenyewe; bali ni sababu miongoni mwa sababu, haina athari yoyote isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka. 4- Iiepukane na ushirikina, au haramu, au uzushi, au yenye kupelekea katika hayo.

Kumethibitishwa madhara ya kijicho, na kwamba ni kweli, inatakiwa kujisomea kutokana na kijicho.

Ni sunna kujifanyia kisomo kupitia yale yaliyokuja katika hadithi.

Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kama watu wengine, humtokea yale yanayowatokea watu wengine, kama maradhi.

Ulinzi wa Mwenyezi Mungu kwa Nabii wake na kumuhifadhi kwake, na kumuwekea kwake Malaika kwa ajili ya hilo.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih Muslim · Hadith Na. 2186 (Fiqhi, Swala na Ibada · Hukumu za Swala na Tohara)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Imepokelewa Imamu Muslim
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
muslim:he:5650