Nyuma

Kutoka kwa Abdillah bin Mas'udi -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Shikamaneni na ukweli, kwani ukweli hupelekea katika wema, na hakika wema hupelekea katika pepo

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ عَبْدِ اللهِ بنِ مَسعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «عَلَيْكُمْ بِالصِّدْقِ، فَإِنَّ الصِّدْقَ يَهْدِي إِلَى الْبِرِّ، وَإِنَّ الْبِرَّ يَهْدِي إِلَى الْجَنَّةِ، وَمَا يَزَالُ الرَّجُلُ يَصْدُقُ وَيَتَحَرَّى الصِّدْقَ حَتَّى يُكْتَبَ عِنْدَ اللهِ صِدِّيقًا، وَإِيَّاكُمْ وَالْكَذِبَ، فَإِنَّ الْكَذِبَ يَهْدِي إِلَى الْفُجُورِ، وَإِنَّ الْفُجُورَ يَهْدِي إِلَى النَّارِ، وَمَا يَزَالُ الرَّجُلُ يَكْذِبُ وَيَتَحَرَّى الْكَذِبَ حَتَّى يُكْتَبَ عِنْدَ اللهِ كَذَّابًا».

Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: Kutoka kwa Abdillah bin Mas'udi -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Shikamaneni na ukweli, kwani ukweli hupelekea katika wema, na hakika wema hupelekea katika pepo, na hatoacha mtu kuwa mkweli na akishughulika na ukweli mpaka ataandikwa kwa Mwenyezi Mungu kuwa ni mkweli, na tahadharini na uongo, kwani uongo unapelekea katika uovu, na hakika uovu hupelekea katika moto, na hatoacha mtu kuendelea kuwa muongo, na akishughulika na uongo mpaka ataandikwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuwa ni muongo".

‘Abdullah ibn Mas‘ūd (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Adhere to truthfulness, for truthfulness leads to righteousness, and righteousness leads to Paradise. A man will keep telling the truth and strive to tell the truth until he is recorded with Allah as the most truthful. Beware of lying, for lying leads to wickedness and wickedness leads to Hellfire. A man will keep telling lies and strive to tell lies until he is recorded with Allah as a persistent liar."

Ukweli ni tabia adhimu ambayo hupatikana kupitia juhudi, kwa sababu mtu anapoendelea kuwa mkweli na kuutafuta ukweli, mpaka ukweli unakuwa ni kama tabia yake ya asili, basi huandikwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuwa ni miongoni mwa wa watu wakweli na wema.

Uongo ni tabia ya kulaumiwa ambayo mhusika huipata kupitia mazoea ya muda mrefu katika maneno na matendo, mpaka inakuwa ni tabia na silika yake, kisha anaandikwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuwa ni katika waongo.

Ukweli unahusu ukweli wa ulimi, ambao ni kinyume cha uongo, na ukweli katika nia, ambao ni ikhlasi, na ukweli katika kusuluhisha vyema nia yake, na ukweli katika vitendo, na kwa uchache zaidi ni siri yake na dhahiri yake viwe sawa, na ukweli katika matukio kama kusema ukweli wakati wa hofu na raha, na mengineyo, hivyo yeyote atakayesifika na sifa hizo basi atakuwa ni mkweli mno, au akasifika na baadhi yake atakuwa mkweli pia.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih Muslim · Hadith Na. 2607 (Maadili, Adabu na Tabia Njema · Wema, Uadilifu na Tabia Njema)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
muslim:he:5504