Nyuma

Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba (unipe) kutoka katika heri zote: zile za haraka na za kuchelewa, kwa ninayo yajua na nisiyo yajua, na ninajikinga kwako kutokana na shari zote zinazokuja haraka na zinazochelewa

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنينَ رضي الله عنها أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَّمَهَا هَذَا الدُّعَاءَ: «اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ الْخَيْرِ كُلِّهِ، عَاجِلِهِ وَآجِلِهِ، مَا عَلِمْتُ مِنْهُ وَمَا لَمْ أَعْلَمْ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ الشَّرِّ كُلِّهِ، عَاجِلِهِ وَآجِلِهِ، مَا عَلِمْتُ مِنْهُ وَمَا لَمْ أَعْلَمْ، اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ خَيْرِ مَا سَأَلَكَ عَبْدُكَ وَنَبِيُّكَ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا عَاذَ بِهِ عَبْدُكَ وَنَبِيُّكَ، اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْجَنَّةَ، وَمَا قَرَّبَ إِلَيْهَا مِنْ قَوْلٍ أَوْ عَمَلٍ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ النَّارِ، وَمَا قَرَّبَ إِلَيْهَا مِنْ قَوْلٍ أَوْ عَمَلٍ، وَأَسْأَلُكَ أَنْ تَجْعَلَ كُلَّ قَضَاءٍ قَضَيْتَهُ لِي خَيْرًا».

Kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimfundisha dua hii: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba (unipe) kutoka katika heri zote: zile za haraka na za kuchelewa, kwa ninayo yajua na nisiyo yajua, na ninajikinga kwako kutokana na shari zote zinazokuja haraka na zinazochelewa, kwa ninayo yajua na nisiyo yajua. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba (unipe) miongoni mwa heri alizo kuomba mja wako na nabii wako, na ninajikinga kwako (uniepushe) na shari alizo jikinga kwako mja wako na nabii wako. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba pepo, na yaliyo karibu yake miongoni mwa kauli au matendo, na ninajikinga kwako kutokana na moto na yaliyo karibu na moto miongoni mwa kauli au matendo, na ninakuomba ujaalie kila hukumu utakayo hukumu kwangu iwe ni heri"

‘Ā’ishah, Mother of the Believers (may Allah be pleased with her), reported that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) taught her this supplication: "O Allah, I ask You for all that is good, the immediate and the deferred thereof, what I know and what I do not know. And I seek refuge with You from all that is evil, the immediate and the deferred thereof, what I know and what I do not know. O Allah, I ask You for the good that Your slave and Prophet asked You for, and I seek refuge with You from the evil that Your slave and Prophet sought refuge from. O Allah, I ask You for Paradise and what brings one closer to it of words or deeds, and I seek refuge with You from the Fire and from what brings one closer to it of words or deeds, and I ask You to make every decree that You have decreed for me good."

Mtu anatakiwa kuifundisha familia yake yale yenye kuwanufaisha katika mambo ya dini na dunia, kama Mtume rehema na amani ziwe juu yake alivyomfundisha Aisha.

Kilicho bora kwa muislamu ni kuhifadhi dua zilizopokelewa kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake; kwa sababu ni katika dua zilizokusanya kheri zote.

Wanachuoni wanasema kuhusu hadithi hii: Ni hadithi iliyokusanya kila kitu katika kuomba kheri na kuomba kinga dhidi ya shari, hii ni katika maneno mafupi yenye maana pana aliyopewa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

Miongoni mwa sababu za kuingia peponi baada ya rehema ya Mwenyezi Mungu: Ni matendo na kauli njema.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sunan Ibn Majah · Hadith Na. HE-5487 (Maadili, Adabu na Tabia Njema · Wema, Uadilifu na Tabia Njema)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Imepokelewa na Ibn Majah na Ahmad
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
ibnmajah:he:5487