Nyuma

Si miongoni mwetu atakayepiga mashavu, na akachana mifuko, na akaomboleza kwa maombolezo ya watu wa zama za ujinga

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَيْسَ مِنَّا مَنْ لَطَمَ الخُدُودَ، وَشَقَّ الجُيُوبَ، وَدَعَا بِدَعْوَى الجَاهِلِيَّةِ».

Imepokelewa kutoka kwa Abdallahi bin Masudi -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Si miongoni mwetu atakayepiga mashavu, na akachana mifuko, na akaomboleza kwa maombolezo ya watu wa zama za ujinga".

‘Abdullah ibn Mas‘ūd (may Allah be pleased with him) reported: The Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "He is not one of us who slaps the cheeks, splits the collars, and calls out with the calls of Jāhiliyyah (pre-Islamic era of ignorance)."

Kemeo lililokuja katika hadithi hii linaonyesha kuwa matendo haya yote ni katika madhambi makubwa.

Ulazima wa kuwa na subira katika msiba, na uharamu wa kuchukizwa na kadari za Mwenyezi Mungu zenye kuumiza, na kulidhihirisha hilo: Kwa kulia kwa malalamiko au makelele au kunyoa, au kuchana nguo au mengineyo.

Uharamu wa kuwaiga watu wajinga kwa mambo yao ambayo sheria imeyathibitisha kwao.

Hakuna tatizo kuhuzunika na kulia, kwani hili halipingani na subira juu ya makadirio ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, bali ni huruma aliyoiweka Mwenyezi Mungu katika nyoyo za ndugu wa karibu na vipenzi.

Ni lazima kwa muislamu kuridhia maamuzi ya Mwenyezi Mungu, na asiporidhia basi kusubiri ni wajibu.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih Muslim · Hadith Na. HE-5380 (Aqidah na Misingi ya Imani · Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
muslim:he:5380