عَنْ أَبِي سَعِيدٍ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَا مِنْ مُسْلِمٍ يَدْعُو بِدَعْوَةٍ لَيْسَ فِيهَا إِثْمٌ، وَلَا قَطِيعَةُ رَحِمٍ، إِلَّا أَعْطَاهُ اللهُ بِهَا إِحْدَى ثَلَاثٍ: إِمَّا أَنْ تُعَجَّلَ لَهُ دَعْوَتُهُ، وَإِمَّا أَنْ يَدَّخِرَهَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ، وَإِمَّا أَنْ يَصْرِفَ عَنْهُ مِنَ السُّوءِ مِثْلَهَا» قَالُوا: إِذنْ نُكْثِرُ، قَالَ: «اللهُ أَكْثَرُ».
Imepokelewa kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakuna muislamu yeyote ataomba maombi yasiyokuwa ndani yake na kuomba dhambi wala kukata udugu, isipokuwa Allah atampa kwa maombi hayo moja kati ya mambo matatu: Moja ima amuharakishie maombi yake, au amlimbikizie ili amlipe siku ya Kiyama, au amuondoshee katika mabaya mfano wake" Wakasema: (Maswahaba) kwa hiyo tuzidishe? Akasema: "Allah ni mwenye kuzidisha mara dufu".
Abu Sa‘īd (may Allah be pleased with him) reported that the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "No Muslim invokes Allah with a supplication that does not involve sin or severing ties of kinship, except that Allah will grant him one of three: either His supplication will be answered soon, or He will save it for him in the Hereafter, or He will avert from him an equivalent amount of evil." They said: Then we should do more. He said: "Allah is even more."
Dua ya muislamu hujibiwa hairejeshwi lakini kwa sharti zake na adabu zake; ndio maana inampasa mja akithirishe dua na wala asitake haraka ya kujibiwa.
Kujibiwa dua hakufungamani na kupata kilichoombwa; kwani anaweza kumfutia madhambi kwa dua yake, au akamlimbikizia Akhera.
Amesema bin Bazi: Kung'ang'ania, na kumdhania vizuri Mwenyezi Mungu, na kutokata tamaa, hizi ni miongoni mwa sababu kubwa za kujibiwa, ni juu ya kila mtu kung'ang'ania katika dua, na awe na dhana nzuri na Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na Kutukuka, na ajue kuwa yeye ni mwenye hekima na mjuzi, anaweza kuharakisha majibu kwa hekima, na anaweza kuyachelewesha kwa hekima, na anaweza kumpa muombaji kitu bora kuliko alichoomba.