Nyuma

Alifaradhisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakatul-fitiri kibaba cha tende, au kibaba cha ngano, kwa mtumwa na aliyehuru, na mwanaume na mwanamke, na mdogo na mkubwa katika waislamu, na akaamrisha itolewe kabla ya watu kutoka kwenda katika swala

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: فَرَضَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ زَكَاةَ الفِطْرِ صَاعًا مِنْ تَمْرٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ شَعِيرٍ، عَلَى العَبْدِ وَالحُرِّ، وَالذَّكَرِ وَالأُنْثَى، وَالصَّغِيرِ وَالكَبِيرِ مِنَ المُسْلِمِينَ، وَأَمَرَ بِهَا أَنْ تُؤَدَّى قَبْلَ خُرُوجِ النَّاسِ إِلَى الصَّلاَةِ.

Imepokelewa kutoka kwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema: Alifaradhisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakatul-fitiri kibaba cha tende, au kibaba cha ngano, kwa mtumwa na aliyehuru, na mwanaume na mwanamke, na mdogo na mkubwa katika waislamu, na akaamrisha itolewe kabla ya watu kutoka kwenda katika swala.

Ibn ‘Umar (may Allah be pleased with him and his father) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) enjoined Zakat al-Fitr as one Sā‘ of dates or one Sā‘ of barley on the slave and the free person, the male and the female, the young and the old from among the Muslims. He ordered that it be given before the people go out to the prayer.

Zakatul-fitiri ya Ramadhani ni lazima kutolewa kwa mtoto na mkubwa, na aliye huru na mamluki, na anasemeshwa hapa msimamizi na bosi, na anaitoa mwanaume kwa niaba yake na watoto wake na wale ambao ni wajibu kwake kuwahudumia.

Si wajibu zakatul-fitiri kwa kichanga kilichoko tumboni, bali inapendeza tu.

Kumebainishwa kinachotolewa katika zakatul-fitiri, nakuwa ni chakula cha watu walichokizoea.

Uwajibu wa kuitoa kabla ya swala ya Iddi, na bora zaidi iwe asubuhi ya siku ya Iddi, na inafaa kuitoa kabla ya Iddi kwa siku moja au mbili.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih Muslim · Hadith Na. HE-4520 (Fiqhi, Swala na Ibada · Hukumu za Swala na Tohara)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
muslim:he:4520